Mh. Mchengerwa azindua Bodi ya BMT, atema cheche, aitwisha mambo matatu
Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameitaka Bodi ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) aliyoiteua hivi karibuni, kuifanya michezo nchini kuwa biashara badala ya kuendelea na mazoea ili kutoa ajira na kuchangia kwenye uchumi wa nchi. Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Aprili 20, 2022 kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam wakati aikizindua rasmi Bodi hiyo ya 15 ya BMT ambapo amefafanua kuwa kazi kubwa ya Bodi hiyo ni kuisaidia Serikali kuandaa timu bora za taifa katika michezo mbalimbali ili ziendelee kufanya vizuri katika michezo kimataifa. Ameitakia Bodi hiyo kuwa na mikakati kabambe ya kuwashirikisha wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali kuja kuwekeza kwenye miundombinu ya michezo ili kuhakikisha kuwa michezo inapiga hatua. Aidha, Mhe. Mchengerwa ameiagiza Bodi mambo mahususi matatu ili kuendeleza michezo nchini huku akisisitiza kuwa mwamko uliopo leo kwenye michezo ni maono na Jitihada zil...

Comments
Post a Comment