Posts

Mhe. Mchengerwa ahimiza kumuenzi Bibi Titi

Image
  Na John Mapepele Waziri Wa Utamaduni, Sanaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amehimiza umuhimu wa kumuenzi mwanaharakati  mwanamke, Bibi Titi Mohamed aliyefanya kazi kwa karibuni na Mwalimu Julisu Nyerere katika harakati za kuleta uhuru wa Tanganyika. Akizungumzia tamasha  la Bibi Titi Mohamed litakalofanyika  wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, Mhe. Mchengerwa kwenye kipindi cha 360 cha kituo cha televisheni cha Clouds leo ambapo amesema  Bibi Titi ni alama ya mabadiliko katika suala zima la ushiriki wa wanakwake katika harakati hizo na kuleta mabadiliko.  “Ukimzungumzia Bibi Titi Mohamed unazungumzia alama ya mabadiliko, unazungumia alama ya kutoka kutoamini kuja katika kuamini kwa sababu Bibi Titi  mwenyewe aliamini kwamba tunaweza kujikomboa,” amesema. Amesema ni vigumu kuzungumzia mabadiliko ya kisiasa ya kuwaingiza wanawake katika siasa, ushawishi wa katika siasa, uchumi, matumizi ya Kiswahili,  bila kumzungumzia Bibi Titi Mohamed.   Amesema...

Mhe. Mhengerwa -Tamasha la Sanaa Bagamoyo ni la kimataifa, Makamu wa Rais afafanua kuwa Sanaa inaongoza katika ukuaji wa uchumi nchini

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema  Serikali imefanya  maboresho makubwa   kwenye Tamasha la mwaka huu la 41 la Utamaduni na Sanaa   Bagamoyo kuwa la kimataifa ambapo limeshirikisha nchi mbalimbali duniani ili kuitangaza Tanzania na utamaduni wake duniani. Kauli hiyo ameitoa leo wakati akimkaribisha Makamu wa Rais Mhe, Dkt. Philipo Mpango kuzindua rasmi tamasha hili kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano. Mhe. Samia  Suluhu Hassan. Ameongeza kuwa tamasha hili limeshirikisha vikundi vya wasanii kutoa mataifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Canada, Zambia, Burundi na Visiwa vya Mayote kutoka nchini Ufaransa. “Mwaka huu tumeendelea  kuliboresha Zaidi tamasha hili kutoka kuwa tamasha la mazoea la wanafunzi wa sanaa hapa chuoni ili kulipatia hadhi zaidi ya kuwa tamasha la kimataifa.” Amesisitiza Mhe. Mchengerwa Aidha amesema wameteleza maelekezo ya Mhe. Rais ya kutaka kuendeleza tamasha hili n...

Mhe. Kikwete aipongeza Wizara kwa kukuza Sekta ya Sanaa kwa kasi, adai ina mchango mkubwa kwenye uchumi

Image
  Na John Mapepele Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza   Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo  kwa  kazi kubwa inayoifanya   ambayo imesababisha kuwa miongoni mwa sekta zinazokuwa kwa kasi na kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye uchumi wa Taifa kwa ujumla. Mhe. Kikwete ameyasema haya Usiku wa kuamkia leo Novemba 6, 2022 akiwa Mgeni wa rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ya Ommy Dimpoz iitwayo Dedication mara baada ya kukaribishwa kutoa hotuba yake na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye amekuwa mgeni wa heshima kwenye uzinduzi huo. Amefafanua kuwa katika awamu hii ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan tasnina ya muziki wa kizazi kipya imekua kwa kasi na kupata mafanikio makubwa ukilinganisha awamu zilizopita.    “Kila siku nikiangalia kwenye televisheni naona wanamuziki na wasanii wapya hali ambayo ina...

Waziri Mchengerwa atoa siku 30 kwa BMT kutengeneza mifumo ya kusajili ya kielektoniki

Image
  Na John Mapepele  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amelielekeza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuhakiksha ndani ya mwezi mmoja linatengeneza mfumo wa kieletroniki wa kusajili vyama vya michezo ili kuondoa usumbufu kwa wadau unaojitokeza. Mhe. Mchengerwa ameyasema  haya  leo Oktoba 27, 2022 wakati akizindua program ya “Mpira Fursa” inayoratibiwa na Taasisi ya Karibu Tanzania (KTO) na kugawa  vifaa vya michezo kwa  Vyuo vya Wananchi vya  Maendeleo 54 kote nchini na shule za msingi 86.   Ameutaka uongozo wa shule ambazo zitabahatika kupata vifaa vya soka, kuwaruhusu wasichana kucheza soka na kuvitumia vifaa hivyo kwa uangalifu na kwa madhumuni yaliyokusudiwa.   Ameipongeza KTO kwa kuanzisha program hiyo ya kupeleka  michezo  katika vyuo vya  wananchi  vya maendeleo na shule za msingi huku akifafanua kuwa  huo ni utekelezaji wa  maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza...

Waziri Mchengerwa azindua zoezi la kitaifa la kusaka na kuibua vipaji "mtaa Kwa mtaa."

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni,  Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Oktoba 16, 2022 amezindua  zoezi la  kitaifa la  kuibua na kusaka vipaji  vya Sanaa la "Mtaa kwa Mtaa" eneo la  Ikwiriri wilayani Rufiji, zoezi ambalo litafanyika nchi nzima. Akizindua zoezi hilo katika eneo la Ikwiriri, Mhe. Mchengerwa amesema eneo linalofuata baada ya uzinduzi wa leo ni Mkoa wa Arusha ambapo litafanyika kila mtaa ili kuibua vipaji kwenye sanaa. Amewataka watanzania  wenye vipaji vya Sanaa kujitokeza wakati wa zoezi hilo likiendelea  ili waweze kuendelezwa baada ya kuibuliwa, huku akisisitiza  kauli ya Kipaji chako ndiyo mtaji wako. "Ndugu zangu hii ni ndoto ya Mheshimiwa Rais wetu, Rais anatamani kuona misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere ya kuthamini na kuendeleza Sanaa inaendelezwa ili kuwanufaisha vijana" amesisitiza,  Mhe. Mchengerwa   Amezitaka mamlaka za wilaya na mikoa kote nchini kusai...

Mhe. Mchengerwa- Tanzania na Real Madrid wajadili ushirikiano katika michezo.

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amefanya majadiliano ya awali na uongozi wa juu wa Klabu ya Real Madrid ya Hispania kuhusu kufanya ushirikiano katika kukuza vipaji vya Soka baina ya Klabu hiyo na  Tanzania. Mazungumzo hayo  yamefanyika leo Oktoba 10, 2022 kwa njia ya mtandao ambapo wamejadili  kufanya uwekezaji mkubwa kwenye kuibua vipaji vya wachezaji wachanga na kuwakuza kuanzia kwenye akademi za michezo. Mhe. Mchengerwa amesema Klabu hiyo imekubali  kushirikiana na  Tanzania  kuendeleza vipaji vya vijana ili kuwapata wachezaji bora wa kimataifa  kwa manufaa ya pande zote mbili.  Mbali na kufanya uwekezaji mkubwa katika kuibua vipaji, pia imejadiliwa kushirikiana katika  kutumia michezo kutangaza utalii  wa Tanzania kwa kutumia mitandao mbalimbali ya Klabu hiyo kongwe duniani. Mhe. Mchengerwa amesema Tanzania ina fursa  kubwa  ya kutumia michezo kuitangaza nchi kimataifa ...

RAIS SAMIA AWAPA SALAMU TEMBO WARRIORS, MHE. MCHENGERWA ATOA AHADI NONO WAKISHINDA

Image
  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaipongeza  Timu ya Taifa ya Tembo Warriors kwa kufuzu kombe la Dunia kwa watu wenye ulemavu linalotarajiwa kufunguliwa Septemba 30, 2022 na kuitaka kutanguliza uzalendo na kujituma ili warudi na Kombe nyumbani. Akizungumza kwa njia ya simu kupitia kwa Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi Waziri Mchengerwa amesema Serikali ya Tanzania ipo pamoja na wao katika kila hatua na ndio maana Rais ameridhia viongozi wa Wizara kuambatana nao katika fainali hizo. “Rais na Serikali yenu ipo pamoja na nyinyi, nendeni mkalipiganie Taifa, onesheni uzalendo na kuhakikisha mnarudi na Kimbe nchini na hiyo itakuwa ni zawadi kwake Mhe. Rais na Tanzania kwa ujumla”’ amefafanua Mhe. Mchengerwa. Aidha ameahidi zawadi nono kwa timu hiyo ikiwemo shilingi milioni 40 endapo watafuzu robo fainali, shilingi milioni 80 wakifuzu kucheza nusu fainali na shilingi milioni 100 waki...