Posts

Showing posts from February, 2022

Mhe. Mchengerwa apongeza watanzania kuongoza Kili Marathon 2022

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewapongeza watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mbio za Kilimanjaro Marathon na kuongoza katika mbio hizo tofauti na miaka ya nyuma ambapo mataifa mengine yamekuwa yakiongoza. Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo, Februari 28, 2022 na kufafanua kuwa mwitikio huo mkubwa umetokana na kazi nzuri ambayo iliyofanywa na Rais wa  Samia Suluhu Hassan toka akiwa Makamu wa Rais ambapo aliongoza kuhamasisha riadha na kuanzishwa kwa klabu za mazoezi (jogging clubs) kwenye kila mkoa hapa nchini. Aidha amesema mikakati kabambe iliyowekwa na Serikali ya sasa kwenye Sekta ya michezo inakwenda kuleta mapinduzi makubwa ikiwa ni pamoja na kutoa ajira nyingi kwa wananchi. Katika mashindano hayo mtanzania Alyce Simbu aliongoza  kilomita 42  aliyetumia muda wa 02:16:30 wakati kwenye kilomita 21 nafasi ya kwanza hadi ya tatu zilichukuliwa na watanzania zikiongozwa na Emmanuel Ginniki (01:00:34), akifua...

MHE. GEKUL AELEZA MIKAKATI YA KUKUZA RIADHA KILI MARATHONI

Image
  Na. John Mapepele  Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul amewapongeza waandaji wa mbio za Kilimanjaro Marathoni huku akifafanua kwamba tukio hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Michezo nchini  inayosisitiza ushiriki wa pamoja kati ya Serikali na wadau  katika kuendeleza michezo mbalimbali ikiwemo riadha.  Mhe. Gekul ameyasema hayo leo Februari 27, 2022 wakati akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) ili atoe hotuba yake kwenye kilele cha mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, 2022 kwenye viwanja vya Chuo kikuu cha Ushirika Moshi.  “Sisi familia ya michezo tunajivunia uwepo wa tukio kubwa namna hii linalowaleta pamoja wanamichezo na wapenzi wa riadha kutoka katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi yetu, kipekee niwapongeze Kilimanjaro Premium Lager kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukuza michezo hapa nchini”. Amesema Mhe. Gek...
Image
  Na John Mapepele  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewataka wasanii wanaopanda leo Februari 24,2022 kuiwakilisha Tanzania kwenye Maonesho makubwa ya kimataifa ya Dubai Expo, Mfalme wa Singeli Sholo Mwamba na Mkongwe wa Muziki wa Asili wa Tanzania Mrisho Mpoto kuendelea kutoa burudani ya kukata na shoka ili kuitangaza Tanzania kimataifa.  Mhe. Mchengerwa amesema haya leo Februari 24,2022 wakati ambapo Sholo Mwamba anatarajia kuendelea kuwaipagawisha dunia kwa nyimbi za singeli  majira ya saa 11:00 jioni  kwenye ukumbi wa *Earth Stage* baada ya  kufanya  vizuri kwenye onesho lake  la awali Februari 22, 2022 na kuwaacha  umati uiliofika   kucheza naye huku wengine wakichukua picha kwa ajili ya matumizi yao. “Tunataka Singeli na muziki wa kwetu uiteke dunia ambapo kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeanza  vizuri safari ya mapinduzi makubwa  ya sanaa kwenye anga za kimataifa” amesisitiza Mhe. Mchenge...

MAMA NA MICHEZO

Image
 

SHOLO MWAMBA KUSIMAMISHA DUNIA DUBAI EXPRO LEO, KESHO

Image
  Na. John Mapepele Mfalme wa muziki wa Singeli nchini, Sholo Mwamba pamoja na msanii wa kizazi kipya Saraphina leo Februari 22, 2022 wanatarajia kupanda   na kuionyesha dunia miziki kutoka Tanzania kwenye onesho kubwa duniani la Dubai Expro.  Kwa mujibu wa ratiba ya waandaji wa onesho hilo Sholo  Mwamba  ndiye anayeanza kupanda  majira ya saa 9:30 alasiri  na Saraphina anapanda  majira ya saa 10:30 jioni ambapo wote watapanda kwenye ukumbi wa Sea Stage. Akizungumza kutoka Dubai, muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani Sholo Mwamba amesema atahakikisha kupitia shoo ambazo anazozifanya, Singeli inakwenda kuwepo kwenye sura ya dunia. Ameongeza kuwa muziki wa Singeli una nafasi kubwa ya kuitambulisha Tanzania na kuvutia watalii wengi kuja kutembelea, hivyo atahakikisha wageni watakaohudhuria onesho hilo wanavutiwa  na muziki huo.  Sholo amepangiwa kutumbuiza mara tatu kwenye onesho hilo leo, kesho Februari 23, majira ya saa 10: 30 jioni w...

Mhe. Mchengerwa awaalika wananchi Tamasha la Serengeti

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa wananchi wote kushiriki kwenye tamasha kubwa Tanzania na Afrika la Muziki la Serengeti (Serengeti Music Festival) litakalofanyika Machi 12, 2022 jijini Dodoma ili kujionea hazina ya vipaji vya wasanii nchini. Mhe. Mchengerwa amesema haya, hivi karibuni jijini Dar es Salaam ambapo amefafanua kuwa tamasha hili ndiyo tamasha kubwa linaloratibiwa na Serikali likiwa na lengo la kuibua vipaji vya wasanii pia kutangaza vivutio vilivyopo nchini ili kuliingizia taifa mapato kutokana na hazina ya utalii uliopo.  Aidha, amesema tamasha hilo litahusisha wasanii zaidi ya hamsini wa miziki ya aina mbalimbali ambao watatumbuiza   ili kuleta vionjo na radha tofauti tofauti.  “Tamasha hili linaleta muunganiko wa kipekee kabisa linaloonyesha tasnia ya burudani na utalii na ndiyo maana tumetumia jina la Mbuga yetu bora Afrika na duniani ya Serengeti ili kuwavutia wageni kutoka sehemu m...

MAELEKEZO YA MHE. MCHENGERWA YAFIKIA PAZURI

Image
  Na. John Mapepele  Maelekezo ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ya kutaka mchakato wa mwaka huu wa utoaji wa Tuzo za Muziki  bila upendeleo  yamefika  mahali pazuri. Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Matiko Mniko, leo Februari 21, 2022 imeeleza kuwa jumla ya kazi 402 zimewasilishwa kuanzia Februari 9, 2022 baada ya zoezi la kuwaelimisha wadau kukamilika na kuwa BASATA limeamua kuongeza muda wa siku saba ili kutoa nafasi kwa wasanii wengi kushiriki. “Tunaongeza siku 7 kwa ajili ya wasanii kuwasilisha kazi katika vipengele vya Tuzo za Muziki Tanzania (TMA 2021)” imefafanua taarifa hiyo.  Pia taarifa hiyo imefafanua kwamba mwisho wa kuwasilisha kazi hizo ni Machi mosi mwaka huu kupitia link www. tanzaniamusicawards.info  Akizungumza kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Utoaji wa Tuzo za Muziki na Ugawaji wa Mirahaba kwa Wasanii Januari 28, 2022 kwenye Ukumbi wa kimataifa wa Julius Nye...
Image
  Na. John Mapepele Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul amezitaka Halmashauri zote nchini kuhamasisha programu ya kufanya mazoezi kuanzia ngazi ya mtaa ili kuimarisha afya kwa jamii na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kuibua vipaji vya michezo kuanzia ngazi ya chini. Mhe. Gekul amesema hayo leo Februari 20, 2022, alipokua Mgeni Rasmi kwenye kilele cha Bonanza kubwa lililoandaliwa na Umoja wa Vilabu vya jogging klabu Mbagala, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza mbio za takribani kilomita 7.5 kuanzia Mbagala hadi Mtoni Kijichi. Amezitaka Klabu za Mazoezi kote nchini kuhakikisha zinashirikisha kikamilifu makundi maalum ya jamii kwenye siku za mazoezi, huku akitoa pongeza kwa umoja wa Mbagala Jogging Klabu kwa kuandaa tamasha hilo ambalo amelielezea kuwa limekuwa la mafanikio makubwa. Aidha, ametoa wito kwa wananchi wote kutenga muda kila siku kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao. “Akina mama wenzangu ujanja ...
Image
  Na. John Mapepele Waziri wa utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Februari 15, 2022 amekutana na Balozi wa Morocco nchini Mhe. Zakaria Elgoumiri na kufanya mazungumzo ya kuendeleza sekta za michezo, utamaduni na Sanaa ambapo  Balozi amesisitiza serikali yake ipo tayari kushirikiana na Tanzania kwa faida ya wananchi wa nchi hizo. Mhe. Mchengerwa amesema Serikali ya Tanzania na Morocco zimekuwa na uhusiano mzuri katika sekta  hizo  toka  muda mrefu  hali ambayo  imewafanya  viongozi wakuu wa nchi zote  kufanya ziara na  kubadilishana  uzoefu  wa sekta hizo. Akiwa katika kikao hicho ambacho aliambatana na Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi, Mkurugenzi wa michezo nchini Yusufu Singo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT) Neema Msitha wamekubalina  na ujumbe wa Mhe. Balozi wa kuendelea kushirikiana  kwenye sekta  hizo.  Ameyataja  baadhi ya maen...

MCHENGERWA AIPONGEZA WASAFI KWA KUKUZA VIPAJI VYA WASANII

Mhe. Mchengerwa apongeza ubunifu wa wadau wa tamasha la Sauti za Busara

Image
  Na. John Mapepele  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewapongeza  wadau mbalimbali wa Sanaa walioshiriki kwenye tamasha la Sauti za Busara Zanzibar kwa ubunifu wao na  kuwataka waendelee kutumia  matamasha hayo kutangaza  bidhaa na huduma wanazozitoa. Mhe. Mchengerwa  ametoa wito huo alipotembelea   mabanda yaliyokuwa yakionesha bidhaa na huduma zao kwenye kilele cha Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Februari 13, 2022. Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotions, Mhe. Simai Mohamed Said ambao ndiyo waandaaji wa tamasha hilo amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa kutembelea wadau wa  tamasha hilo huku akisisitiza kuwa  kitendo hicho kimeonesha anathamini mchango wa wadau hao. Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotion, Sinai Mohamed Said  akimtambulisha Mhe. Mchengerwa kwa mmoja wa wadau kwenye banda la Benki ya CRDB Mhe. Mchengerwa akiwa na kikosi cha mfalme wa Singeli nchini Sholo Mwamba kabla ya kikosi kupan...

Mhe. Mchengerwa aikaribisha dunia Tamasha la Serengeti kupitia Sauti za Busara

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewakaribisha  wageni mbalimbali waliohudhuria tamasha  kubwa  la kimataifa la Sauti za Busara  kutoka  sehemu  mbalimbali duniani kushiriki kwenye  tamasha la kihistoria  la muziki la Serengeti litakali fikia kilele chake Machi 12, mwaka  huu jijini Dodoma. Akizungumza kwenye kilele  cha Tamasha la Sauti za Busara usiku wa kuamkia leo  Februari 14, 2022 huko zanzibar amesema  Serikali inakwenda  kuandaa matamasha makubwa  ya kihistoria ambayo yataonesha  utamaduni wa  kitanzania, hivyo dunia inakaribishwa kushuhudia tukio hili la kihistoria na kimataifa. "Naomba kutumia nafasi hii  kuwakaribisha  kwenye  Tamasha la Serengeti na Tamasha la kimataifa la Sanaa na Utamaduni  la Bagamoyo ambayo yanakwenda  kuionyesha dunia  utajiri wa utamaduni  na vivutio vya utalii duniani". Ameongeza Mhe....
Image
   Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Mohamed Mchengerwa amemtembelea  aliyekuwa Mbunge wa Mikumi na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Bw. Joseph Haule (Prof. Jay) anayetibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.   Mhe. Mchengerwa amefika leo Februari 12, 2022 kumjulia hali msanii huyo  na kuwasilisha salamu za Serikali kama msimamizi Mkuu wa Sekta ya Sanaa hapa nchini. “Nimefika kumjulia hali mmoja wa wadau na miongoni mwa wasani ambao tunatambua na kuthamini  mchango wa kazi zake za sanaa ambazo zimehamasisha vijana wengi kujiajiri kupitia Sanaa ya muziki hapa nchini". Ameeleza Mhe. Mchengerwa Tayari  Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema itagharamia matibabu yake hadi hapo ataporuhusiwa kutoka hospitalini hapo. Kwa upande wake mke wa Prof. Jay, Bi. Grace Mgonjo amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa upendo wa kuja kumwona msanii huyo . Pia ameushukuru Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili  kuwapokea na kuwahudumia...

MHE. MCHENGERWA AELEZA NAMNA RAIS SAMIA ALIVYOIBEBA TASNIA YA FILAMU NCHINI

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Omary Mchengerwa amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuweka mazingira wezeshi ya kuendesha shughuli za sanaa na michezo nchini kwa kuchukua hatua mbalimbali za kimkakati ambazo zimeanza kuzaa matunda  katika kipindi kifupi.  Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo, Februari 12, 2022 kwenye dhukuru na wadau wa tasnia ya Filamu iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa dhamira yake pia ni kuona sekta ninazozisimamia zinapiga hatua kubwa za kimaendeleo, na kuleta mapinduzi makubwa ambayo hayajawai kutokea.  Ametaja baadhi ya mazingira wezeshi ambayo Mhe. Samia ameyaweka katika kipindi hiki kuwa ni pamoja na kuandaa filamu ya Royal Tour inayolenga kuitangaza Tanzania katika Nyanja mbalimbali za uwekezaji ikiwemo katika sekta ya filamu ambayo yeye mwenyewe ameshiriki kikamifu katika filamu hiyo.   Pia amesema Mhe. Rais ameridhia kutenga fedh...

MHE. MCHENGERWA KUFANYA DHUKURU NA WADAU WA FILAMU

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa kesho Februari 12, 2022 ataanza kufanya dhukuru na wadau wa sekta ya Filamu jijini Dar es Salaam ikiwa ni mkakati wa makusudi wa kufanya tafakuri ya pamoja na wadau mbalimbali wa sekta anazoziongoza ili kutatua changamoto zinazowakabili na kuleta mapinduzi ya haraka. Haya yameelezwa leo Februari 11, 2022 na Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi wakati akizindua rasmi Tamasha la Muziki la Serengeti jijini Dar es Salaam. Amesema kundi la kwanza analokutana nalo kesho litahusisha wadau mbalimbali wa filamu ambao ni pamoja na watayarisha,waongozaji, wapiga picha, waandika miswada, waigizaji, wahariri na  walimu kutoka shirikisho la filamu. Akizungumza alipotembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) hivi karibuni Mhe. Mchengerwa amelielekeza TaSUBa na wadau mbalimbali wakiwemo wazalishaji wa muziki hapa nchini kuandaa muziki wa kitanzania ambao utalitambulisha t...

MHE. MCHENGERWA AAGIZA BAKITA KURATIBU SIKU YA KISWAHILI DUNIANI KIMKAKATI

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameliagiza Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kuratibu Siku ya Kiswahili Duniani kwa kushiriana na Wizara ya Mambo ya Nje na wadau mbalimbali ikiwa ni mkakati wa makusudi wa kuibidhaisha lugha hiyo duniani.  Kauli hiyo ameitoa leo Februari 9, 2022 jijini Dar es Salaam kwenye Ofisi za BAKITA alipotembelea, kukagua shughuli za BAKITA kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa kuwa Waziri mwenye dhamana Utamaduni, Sanaa na michezo ambapo pia ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara yake Dkt. Hassan Abbasi. Amesema kwa vile siku hii imetambuliwa duniani na imeshatangaza kuwa lugha ya kazi kwenye Umoja wa Afrika ni lazima kuipa umuhimu wa kipekee na kuiandaa kwa kuitangaza kwa nguvu zote ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kimkakati ambapo ametaka kila ubalozi wa Tanzania duniani kuadhimisha siku hii kikamilifu. Akifafanua amesema maandalizi hayo yanatakiwa kuhusisha wadau wote ambao kwa namna moja au nying...